Picha : Mwonekano wa Soko kuu Njombe Mji

0
157

Mwonekano wa soko kuu la kisasa la Njombe Mji lenye ukubwa wa mita za mraba 9,186, na ambalo lina sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na maduka 162, meza za biashara 407, migahawa miwili vizimba vya kuku 27 na machinjio ya wanyama wadogo.

Pia soko hilo lina mfumo wa kutambua
viashiria vya majanga ya moto, lina mfumo wa kupambana na majanga ya moto, lina mfumo wa kamera za kiusalama (CCTV Camera system), mfumo wa habari na mawasiliano na sehemu za maengesho ya magari 120 kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa michoro ya usanifu, soko hilo litahudumia wafanyabiashara wasiopungua 630 na ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 10.2.

Rais Samia Suluhu Hassan ambaye yuko katika ziara yake mkoani Njombe, leo anatarajiwa kuzindua soko hilo kuu la kisasa la Njombe Mji.