Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema, ujenzi wa barabara ya Makete – Mbeya utaanza mwezi Septemba mwaka huu, na kwamba mkandarasi ameishapatikana.
Profesa Mbarawa amesema, ujenzi wa barabara hiyo utaanza kwa kipande cha Kitulo hadi Inyuho chenye urefu wa kilomita 36.3.
Amesema ujenzi utaanza na kipande hicho, kwa kuwa sehemu hiyo ni korofi hasa inaponyesha mvua.
Waziri huyo wa Ujenzi na Uchukuzi amesema vipande vinavyofuata wataweka mkandarasi kuanzia Makete wakutane na mkandarasi atakayeanzia ujenzi Mbeya, ili barabara hiyo iweze kuwekewa lami kwa asilimia mia moja.