Mkutano mkuu wa CAF kufanyika kesho

0
122

Maandalizi kwa ajili ya mkutano mkuu wa 44 wa Shirikisho la kandanda Barani Afrika (CAF) yamekamilika, ambapo wajumbe zaidi ya 150 kutoka mataifa 52 ya bara hilo wanatarajiwa kushiriki.

Mkutano huo unaofanyika jijini Arusha, Tanzania utahudhuriwa pia na Rais wa FIFA Gianni Infantino kama mgeni maalum.

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua mkutano huo ambao kwa mara ya kwanza unafanyika hapa nchini.