Rungu la TCRA laiangukia ayo TV

0
230

Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeitaka televisheni ya mtandaoni ya Millard Ayo ( ayo TV) kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo, baada ya kuchapisha maudhui yanayoonesha miili ya watoto wa shule ya msingi ya King David, waliofariki dunia katika ajali ya gari mkoani Mtwara hivi karibuni.

Kamati hiyo imetoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza utetezi uliotolewa na ayo TV, ambayo ilikiri kuchapisha maudhui hayo na wayafuta baada ya muda mfupi.

Hata hivyo Kamati hiyo imejiridhisha kuwa utetezi uliotolewa ni hafifu na kujiridhisha kuwa televisheni hiyo imekiuka kanuni ya mawasiliano ya kielektroniki na posta ya maudhui mtandaoni ya mwaka 2022 baada ya picha walizichapisha kuudhi, kuhuzunisha na kudhalilisha marehemu.

Mbali na hilo kamati hiyo pia imekiagiza kituo hicho kuhakikisha kinazingatia utu, kanuni, misingi, sheria na viwango katika uchapishaji na uandaaji wa habari zake, pamoja na kuunda bodi ya wahariri wa taarifa zake.