Rais Samia aweka jiwe la msingi VETA Mbarali

0
166

Rais Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Akiweka jiwe hilo la msingi Rais Samia amesema atarudi kuzindua chuo hicho ambacho kitaanza kutoa mafunzo ya muda mfupi mwezi wa Septemba mwaka huu na ya muda mrefu mwezi Januari mwaka 2023.

Chuo hicho ni miongoni mwa utekelezaji wa mkakati wa ujenzi wa vyuo vipya 29 katika wilaya mbalimbali nchini.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Anthony Kasore amesema, vyuo hivyo vinalenga kuwanufaisha wazawa katika kuwajengea uwezo wa kujiajiri.