Mkuu wa Idara ya utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema Jeshi la kujenga taifa linaendelea na mikakati ya kujitosheleza kwa chakula na kutaja moja ya mikakati yake kuwa ni kujikita zaidi katika kilimo cha umwagiliaji.
Brigedia Mabena ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukagua mashamba darasa ya Jeshi hilo katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Amesema Jeshi hilo pamoja na kutumia mbegu bora na kufuata kutoka kwa wataalamu ili kujitosheleza kwa chakula hawana budi kujikita zaidi katika kilimo cha umwagiliaji ili kuendana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo hadi sasa tayari zipo hekari 2500 za kilimo cha umwagiliaji.