Mwenyekiti wa kamati ya maonesho ya nanenane wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Shija Lupi amesema elimu inayotolewa na Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Mashamba Darasa yaliyopo maeneo yanapoendela maonesho ya siku kuu za nanenane yataendela kuwa endelevu hata baada ya maonesho hayo kufikia tamati.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Jijini Mbeya yanapoendelea maonesho ya Nanenane Kitaifa Katika viwanja vya John Mwakangale hanapoendela maonesho ya sherehe za wakulima maarufu Nanenane.
Amesema lengo la mashamba darasa ni kuhakikisha wananchi wanapata elimu bora ya kilimo na ufugaji kipitia wataalamu wa Jeshi hilo wakati wote na mashamba darasa hayo huwa endelevu kwa kipindi chote cha mwaka.
Kwa upande wake Msimamizi wa mashamba darasa Meja Emmanuell Mwakimage amesema kwa kutumia kanuni bora za kilimo na teknolojia mbalimbali zinazotumiwa na jeshi hilo zimewezesha kupata mazao mazuri katika mashamba hayo hata kipindi cha baridi ambapo hali ya hewa ni changamoto kwa ukuaji wa mazao hayo hivyo wananchi kupitia mashamba hayo wakajifunze ujuzi huo ujuzi.
Naye Mkurugenzi wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Jeshi hilo Kanali Peter Lusika,amesema Jeshi hilo linaendelea kuwapatia wakulima elimu ya teknolojia mbalimbali za kilimo na ufugaji ili waweze kufiki lengo la Serikali ikiwa ni hadi kufika mwaka 2030 Sekta ya kilimo iweze kuchangia asilimia 10 ya pato la taifa.