Rais Samia : Maji yatoke muda wote sio kwa sababu leo nimefika

0
221

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watumishi wa Wizara ya Maji kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji muda wote.

Rais Samia amesema hayo alipokuwa akizindua mradi wa Maji wa Makongolosi uliopo Chunya mkoani Mbeya, mradi ambao utawanufaisha wananchi wa kata ya Makongolosi na Bwawani.

“Naomba nitoe angalizo, hapa maji yanatoka sasa isije ikawa yanatoka kwa sababu Rais amefika halafu akiondoka hayatoki, naomba isiwe hivyo,” amesema Rais Samia.

Awali akitoa maelezo ya mradi huo mbele ya Rais, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Anthony Sanga amesema mradi huo umefikia 70% ambapo awali uliwafikia wananchi kwa 10% tu.