Rais ateua majaji wapya 22

0
185

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa maafisa 22 kuwa majaji wa Mahakama Kuu.

Kati ya maafisa hao walioteuliwa ni pamoja na Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata; Mwendesha Mashtaka Mfawidhi Mahakama Kuu ya Zanzibar, Haji Suleiman Haji pamoja na Fatma Rashid Khalfan, Kamishna Tume ya Hakiza Binadamu na Utawala Bora.