Mazao ya nyuki kuongezewa mnyororo wa thamani.

0
184

Wafugaji wa nyuki wametakiwa kuzingatia mbinu bora za uzalishaji wa mazao ya nyuki ili kukidhi mahitaji soko la Kimataifa nakuongeza kipato Chao kupitia mazao hayo.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Ofisa Ufugaji Nyuki Mkuu wa Mamlaka ya huduma za Misitu Tanzania TFS Philip Ndilahomba wakati ufunguzi warsha ya siku Tatu Kwa ajili ya kuwajengea uwezo wafugaji,wachakataji na wafanyabiashara wa mazao ya nyuki ili kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya nyuki ili kukidhi soko la Kimataifa

Aidha Ofisa huyo amesema katika Mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwa zikiwemo changamoto zinazowakumba ww pamoja na viwango vya ubora wa mazao ya nyuki na mazingira ya kuzalishia asali hadi kumfikia mlaji wa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Ofisa wa Viwango wa Shirika la Viwango Tanzania TBS Fatuma Mauniko amewataka wazalishaji kuzingatia usalama katika uzalishaji wa bidhaa wanazozalisha ili kujiongezea fursa ya masoko ya nje yenye uhakika.

Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wamesema kutolewa Kwa Semina hiyo kutawasaidia kitatua changamoto mbalimbali kwenye Ufugaji wa nyuki na usafirishaji wa asali.

Takribani Wilaya kumi na nane zinatarajiwa kunufaika na mafunzo hayo Tanzania Bara na Visiwani.