Chongolo : Zoezi la sensa si la kisiasa

0
124

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema zoezi la sensa ya watu na makazi si la kisiasa, bali ni la maendeleo ya watanzania wote hivyo wajitokeze kuhesabiwa.

Chongolo ametoa kauli hiyo hii leo katika kata ya Kaloleni wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, alipozungumza na wanachama wa CCM wa Shina namba mbili.

Akihamasisha wananchi kushiriki sensa ya watu na makazi inayofanyika tarehe 23 mwezi huu Chongolo amesema, sensa sio suala la kisiasa na kuonya wanachama wa CCM na wananchi wasikubali kuhadaiwa.

Chongolo yupo katika ziara ya kukagua uhai wa Chama Cha Mapinduzi mkoani Kilimanjaro.

Pia anatumia ziara hiyo kuhamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi.