Tanzania haina homa ya Nyani

0
171

Mganga Mkuu wa serikali Dkt. Aifello Sichalwe amesema, mpaka sasa hakuna mgonjwa aliyethibitika kuugua homa ya Nyani hapa nchini.

Dkt. Sichalwe ametoa kauli hiyo mkoani Manyara, alipokuwa
akizungumza na wataalamu wa afya wilayani Babati.

Amesema kumekuwa na maswali mengi yanayoonesha baadhi ya wananchi wana hofu kuhusu homa hiyo ya nyani, lakini serikali inafuatilia kwa taarifa za kila mgeni anayeingia nchini ambapo hadi sasa hakuna mgonjwa wa homa hiyo.

Dkt. Sichalwe amewataka Watanzania kuchukua tahadhari za ugonjwa huo na kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapoona dalili za ugonjwa wasioufahamu ili serikali ichukue hatua za haraka kudhibiti.

Homa ya Nyani husababishwa na wanyama aina ya Nyani na Panya, ambapo mgonjwa huwa na muonekano wa malengelenge hasa maeneo ya mikono yanayofanana na ugonjwa wa Tetekuanga.