Wanamgambo wa Taliban wamelaani mauaji ya kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa Al – Qaeda, Ayman Al – Zawahiri
yaliyotekelezwa kwa kutumia ndege isiyo na rubani katika mji wa Kabul.
Al -Zawahiri ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji na raia wa Misri, alikuwa katika orodha ya viongozi wa mtandao wa
Al – Qaeda, ambao wanatafutwa na Idara za Ujasusi za Marekani kutokana na kuratibu mashambulio ya kigaidi likiwemo lile lililofanyika Marekani Septemba 11 mwaka 2001.
Marekani iliweka dau la dola milioni 25 milioni za Kimarekani kwa yeyote atakayetoa taarifa ambazo zingefanikisha kukamatwa kwa
Al -Zawahiri , lakini haikuwezekana kwa muda wa miaka saba hadi aliposhambuliwa katika tukio hilo.
Al -Zawahiri alikuwa kiongozi namba mbili wa Al – Qaeda baada ya Osama Bin Laden ambaye naye aliuawa na vikosi vya Marekani.
Kwa muda mrefu tangu kutokea shambulio la Septemba 11, Al – Zawahiri alikuwa mafichoni huko Kabul.