Rais wa Zambia awasili nchini

0
125

Rais Hakainde Hichilema wa Zambia amewasili nchini kwa ziara ya siku moja.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mkoani Dar es Salaam, Rais Hichilema amepokelewa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.

Mapokezi ya Hichilema yalipambwa na burudani iliyotolewa na vikundi mbalimbali.

Pia amekagua gwaride lililoandaliwa rasmi kwa ajili yake, ambapo pia nyimbo za Mataifa yote mawili zilipigwa wakati wa mapokezi hayo pamoja na kupigiwa mizinga 21.

Akiwa hapa nchini, pamoja na mambo mengine Rais Hichilema atakuwa na mazungumzo na mwenyewe wake Rais Samia Suluhu Hassan.

Mazungumzo hayo yatahusu zaidi kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Zambia na ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.