Simba yamaliza “pre Season” kwa ushindi

0
190

Klabu ya soka ya Simba imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya klabu ya Al Kholood ya Saudi Arabia, kwenye mchezo wa mwisho wa kirafiki uliochezwa mjini Ismailia nchini Misri.

Magoli ya Simba yamefungwa na nyota mpya Augustine Okrah na Gadiel Michael, katika mchezo wa nne wa kirafiki kwa klabu hiyo ambayo imeweka kambi kwa wiki tatu nchini Misri.