Kiteto watoa zawadi kwa Rais Samia

0
150

Wanawake wa tarafa ya kijungu wilayani Kiteto mkoani Manyara wametoa zawadi ya kitenge na fimbo ya heshima kwa Raia Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea kituo cha afya.

Serikali inaendelea na ujenzi wa vituo vya afya katika tarafa kupitia fedha za tozo za miamala ya simu.

Kukamilika kwa kituo hicho, kutaondoa adha ya wananchi kutembea kilomita 75 kwenye kupata huduma za afya Hospitali ya Wilaya Kiteto, kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi takribani 31,500.

Akizungumza wakati wa kukabidhi kitenge hicho, mkazi wa tarafa hiyo, Monica Mihambo amesema:” napenda kuwawakilisha wanawake wote wa Kijungu kutoa zawadi hii, wanatoa shukrani zao za dhati kwa kuwaletea kituo cha afya.’

” Hapo awali hatukuwa na kituo cha afya, tulilazimika kutembea kilomita nyingi sana kufuata huduma za afya. Tunaamini ujio wa kituo hiki utasaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa kiasi kikubwa.”

” Tufikishie salamu kwa Mama Rais Samia na hii zawadi kwa kutuletea zawadi ya kituo cha afya kitakachokoa maisha yetu.”

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Innocent Bashungwa alitoa shukrani kwa zawadi na kuahidi kuzifikisha kwa uaminifu mkubwa kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan