Hakuna mgonjwa mpya wa homa ya mgunda

0
156

Wizara ya Afya imesema hadi kufikia leo, idadi ya wagonjwa waliothibitika kuugua homa ya Mgunda (Leptospirosis)
nchini ni 20, na watatu kati yao wamefariki dunia.

Takwimu hizo zimetolewa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, alipokuwa akitoa taarifa kuhusu mwenendo wa homa hiyo ya Mgunda.

Amesema taarifa za ufuatiliaji wa ugonjwa huo kutoka mkoani Lindi zinaonesha kuwa, toka tarehe 18 mwezi huu ilipotolewa taarifa ya ugonjwa huo hakuna mgonjwa mpya aliyeonesha dalili za ugonjwa huu.

Waziri Ummy ameongeza kuwa kwa sasa hakuna mgonjwa aliyelazwa, wote wameruhusiwa kurudi nyumbani.

Amesisitiza kuwa ugonjwa huo unatibika kwa kutumia dawa ambazo zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini.