Kinana akerwa na utitiri wa trafiki barabarani

0
259

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amemsihi Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IJP Camilius Wambura, kufanya tathmini ili kuona kama inawezekana kupunguza idadi ya askari wa usalama barabarani ambao wamekuwa wakilalamikiwa kusababisha kero kwa wananchi.

Kinana ametoa ushauri huo leo akiwa katika mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambapo amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ya mikoa ya Songwe na Mbeya dhidi ya idadi kubwa ya askari wa barabarani ambao wamekuwa wakiwasimamisha mara kwa mara, hivyo kucheleshewesha shughuli za maendeleo.

Mmoja wa wanachama wa CCM ambaye ni dereva wa magari ya kubeba abiria amesema wamechoka kusimamishwa mara kwa mara na matrafiki na kila wanaposimama wanatozwa shilingi 2,000 kwa kila kituo.