Birikau waahidiwa kituo cha afya

0
97

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Mwinyi, amewaahidi wakazi wa eneo la Birikau kuwa atahakikisha anawajengea kituo cha afya ambacho kitakuwa kinatoa huduma ya mama na mtoto katika eneo hilo.
 
Dkt. Mwinyi ametoa ahadi hiyo baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya kuelekea Kijangwani – Birikau unaofadhiliwa na taasisi ya Milele, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoa wa Kusini Pemba.