Manufaa sita ya Sensa ya Watu na Makazi 2022

0
208


Agosti 23 mwaka huu Tanzania itaendesha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambalo hufanyika kila baada ya miaka 10 likilenga kujua idadi ya watu pamoja na taarifa nyingine muhimu kuhusu wananchi.

Lakini Je! Zoezi hili lina umuhimu gani? Haya ni baadhi ya manufaa ya Sensa katika ngazi ya kitaifa na kifamilia.

  1. Kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;
  2. Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;
  3. Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;
  4. Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;
  5. Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na
  6. Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.