Mbeya City yaanza maandalizi ya ligi kuu

0
150

Klabu ya soka ya Mbeya City imeanza maandalizi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu ya soka ya NBC.

Leo imekuwa siku ya pili ya mazoezi ya kikosi hicho maarufu Koma kumwanya ambacho kinajiwinda na msimu mpya wa ligi wa 2022/2023.

Uongozi wa Klabu hiyo umesema hauna mpango wa kufanya mabadiliko makubwa bali kuziba nafasi ambazo zimependekezwa na benchi la ufundi.

Mbeya City inayonolewa na raia wa Uganda Mathias Lule ilimaliza Ligi ya msimu uliopita katika nafasi ya 6.