Anne Makinda: Asiyeeleweka huko awekwe kando

0
140

Kamisaa wa sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022 Anne Makinda amewaasa wakufunzi wa sensa ngazi ya mkoa kuwa makini katika kuwabaini watendaji wengine wenye sifa ya kufundishwa na kuwaweka kando wasiokuwa na sifa.

Makinda ambaye ni Spika mstaafu wa Bunge ametoa kauli hiyo mkoani Dodoma, wakati wa kuhitimishwa kitaifa mafunzo ya sensa ya watu na makazi yaliyotolewa kwa watendaji ngazi ya mkoa.

Baada ya kuhitimishwa mafunzo hayo, watendaji hao watatakiwa kwenda kuwafundisha makarani na watendaji wengine ngazi ya wilaya, kata, vijiji na vitongoji.

Kwa upande wa wananchi, Kamisaa Makinda amewataka kuwa wakweli wanapotoa taarifa za maswali watakayoulizwa na makarani wa sensa, na kusisitiza kuwa taarifa hizo ni kwa ajili ya matumizi ya zoezi la sensa pekee.

Sensa ya watu na makazi itafanyika nchi nzima Agosti 23 mwaka huu.