Mafunzo ya sensa yahitimishwa rasmi kitaifa

0
110

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, amefunga rasmi kitaifa mafunzo ya sensa ya watu na makazi yaliyokuwa yakitolewa kwa wakufunzi ngazi ya mkoa yaliyoendeshwa kwa muda wa siku 21 jijini Dodoma.

Akifunga mafunzo hayo Dkt. Nchemba amewaasa waliopatiwa mafunzo hayo kutumia elimu waliyoipata kukusanya taarifa kwa weledi na umakini, ili
zikatumike kupanga maendeleo ya Taifa.

Amesema mafunzo yaliyotolewa yana lengo la kuwajengea uwezo watendaji wa sensa ya watu na makazi utakaowawezesha kuzifahamu mbinu bora za kukusanya taarifa zitakazofuata vigezo vya Umoja wa Mataifa.

Mbali na kufunga mafunzo hayo, Dkt. Nchemba amewatunuku vyeti wakufunzi bora kitaifa waliohitimu mafunzo ya sensa ya watu na makazi .