Ajali yaua kumi, 8 wanafunzi

0
140

Watu kumi wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotolea mapema hii leo katika eneo la Mjimwema manispaa ya Mtwara – Mikindani mkoani Mtwara.

Taarifa za awali kutoka mkoani Mtwara zinaeleza kuwa miongoni mwa watu waliofariki dunia ni wanafunzi nane wa shule ya msingi ya King David,
dereva wa basi dogo la shule pamoja na mama mmoja anayedaiwa kuwa aliomba lifti kwenye basi hilo.

Wanafunzi wengine 19 wamejeruhiwa katika ajali hiyo, huku watano hali zao zikielezwa kuwa ni mbaya.

Habari zaidi zinaeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo huenda ni kushindwa kufanya kazi vizuri kwa mfumo wa breki wa basi hilo la shule.