Amiri Jeshi Mkuu, Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na ile ya mkuu wa mkoa wa Dodoma, kutafuta eneo utakapojengwa Mnara wa Mashujaa wenye hadhi ya makao makuu ya nchi.
Ametoa agizo hilo mkoani Dodoma wakati wa kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa iliyofanyika katika viwanja vya mashujaa.
Rais Samia amelazimika kutoa agizo hilo kutokana na jiji la Dodoma kuendelea kukua na uwanja huo kuwa katikati ya mji .