EACOP yashusha neema kwa wanaopisha mradi

0
173

Moja ya Wananchi waliopisha Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki EACOP kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania Kazimila Mshandete ameishukuru Serikali Kupitia EACOP kwa kumjengea nyumba nne za kisasa kijijini Sojo na kuishi maisha mapya na ya furaha.

Mshandete amesema awali alikuwa na nyumba duni lakini sasa anafurahia maisha kwenye makazi mapya nje kidogo ya Mradi wa Bomba hilo kijiji cha Sojo Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora na kuwashukuru wasimamizi wa Mradi huo kwa hatua zote walizofata hadi kukamilika kuhamia kwenye makazi mapya.

Aidha Mshandete amesema mbali na kujengewa nyumba hizo EACOP wamewasaidia Wananchi hao kufanya kilimo cha kisasa na kumfanyia kupata mazao mengi zaidi kabla ya kilimo alichokuwa akifanya awali akisema kuwa awali alikuwa akipata gunia 5 kwa msimu akilima, lakini mwaka huu baada amepata gunia 36 kutokana na kulima kisasa kwa msaada wa EACOP

Amesema mbali na kupata elimu ya kulima kisasa pia wamefundishwa kufuga kisasa ambapo anajiandaa kufanya ufugaji wa kuku iliwkujikimu kimaisha na kuongeza kipato chake na familia yake. Anaeleza kuwa Pamoja na kuhamia makazi mapya bado EACOP wanaendelea kuwafuatilia na kujua mahitaji yao ikiwa ni pamoja na kupata chakula Cha kujikimu kutokana na idadi ya familia kila mwezi zoezi litakalodumu kwa miaka 3