Watoka nyumba za nyasi na udongo sasa nyumba za kisasa

0
187

Wananchi wanaopisha Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Kiguzi ambao patakuwa na Kambi kubwa ya Mradi wameendelea kujengewa nyumba za kisasa katika maeneo mapya ikiwepo kijiji cha Kamatojo wilaya Muleba ambako mkandarasi ameendelea kujenga nyumba hizo ili kupisha eneo ambalo bomba hilo litakapopita

Mratibu wa mradi huo, Asiad Mrutu amesema nyumba zinazojengwa ni za kisasa ikiwepo kuwekewa bati za kisasa, umeme, matanki ya maji, stoo na majiko.

Asiad ameongeza kuwa Wananchi waliochagua kujengewa nyumba wamewajengea nyumba karibu na vijiji walivyokuwepo ili waendelee kunufaika na fursa mbalimbali zitakazopatikana kwenye mradi huo mkubwa Afrika Mashariki

Kwa upande wake Afisa Sheria wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Barnabas Mwashambwa amesema waliopisha mradi na kujengewa nyumba zitakapokamilika watahamishiwa kwenye nyumba hizo kwa gharama za mradi huku akisema mikataba inawapa warantii ya miezi 12 endapo kutatokea dorasi kwenye hizo nyumba zitagharamiwa na mkandarasi.

Serikali ya Uganda na Tanzania zimekubaliana kujenga mradi huu wa kimkakati wa EACOP wenye kilomita 1,445 (Tanzania pekee ni 1,147km) kuanzia Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania unaokadiriwa kutumia Dola za kimarekani bilioni 5.1 Sawa na shilingi trilioni 11 hadi kukamilika kwake.