Rais Samia kuongoza maadhimisho ya Siku ya Mashujaa

0
108

Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa, itakayofanyika kitaifa Julai 25, 2022 mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo baada ya kukagua maandalizi ya maadhimisho hayo, katika viwanja vya Mashujaa na kueleza kuridhishwa na maandilizi yaliyofanywa na kamati ya maadhimisho kitaifa kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

“Sherehe hii itafanyika kitaifa mkoani Dodoma na itaongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Viongozi wastaafu na viongozi wengine wa kitaifa.”

Amesema, Rais aliridhia maadhimisho hayo yafanyike kitaifa mkoani Dodoma, lakini akaelekeza yafanyike nchi nzima kwa wakuu wa mikoa kuadhimisha siku hiyo kwa kwenda kwenye maeneo muhimu ya kumbukumbu kwenye mikoa yao.

Katika maadhimisho ya mwaka huu Jeshi la Uhamiaji limeanza kushiriki kikamilifu kwenye gwaride kuanzia kwenye tukio hio muhimu la mashujaa”