Wakurugenzi watakiwa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo

0
105

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo ili waweze kufanya shughuli zao kwenye maeneo rafiki bila bugudha yeyote.

Bashungwa ameyasema hayo wakati akiongea na wafanyabiashara wadogo wadogo wa matunda na mboga mboga kwenye eneo la Mtumbati wilayani Kilosa mkoani Morogoro katika ziara yake ya kikazi wilayani humo.

Amesema wakurugenzi wanapaswa kutenga na kuboresha maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo kuendelea na shuguli zao katika mazingira bora na rafiki.

Aidha, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa kuendelea kutenga na kutoa mikopo kwa wajasariamali wakiwemo wafanyabiashara wa soko la hilo.