Watanzania watesa klabu ya Ajax

0
188

Vijana wa Kitanzania wanaofanya mafunzo ya soka kwenye klabu ya Ajax Amstardam ya Uholanzi chini ya umri wa miaka 15 Giovanni Semaganga na Baraka Seif, leo wamehitimu mafunzo hayo na kutunukiwa medali.

Baraka ametunukiwa medali ya dhahabu ya One V One kwa uwezo wake wa kuwatambua mabeki kwa umri wa chini ya miaka nane, huku Giovanni akitunukiwa medali ya shaba ya One V One kwa vijana chini ya umri wa miaka kumi.