SABA TV kisemeo kipya maudhui ya Afrika

0
206

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha akitoa mhadhara kwa Wakurugenzi wakuu pamoja na Watendaji wakuu wa vyombo vya Habari vya Kusini mwa Afrika (SABA), juu ya umuhimu wa chaneli mpya ya televisheni ya SABA TV inayatarajiwa kuanza kurusha matangazo yenye maudhui ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) hivi karibuni.

Akitoa mhadhara huo kwenye kikao cha bodi ya SABA kinachoendelea nchini Namibia Dkt. Rioba amesema kuwa, SABA TV inakuja kuwa kisemeo cha maudhui yenye mrengo wa Kiafrika.