Biden akutwa na UVIKO-19

0
184

Rais Joe Biden wa Marekani amepimwa na kukutwa na virusi vya UVIKO-19, na hivi sasa amejitenga akiwa Ikulu.

Biden mwenye umri wa miaka 79 ambaye inaelezwa amepata chanjo kamili dhidi ya UVIKO -19 na amepokea dozi ya chanjo hizo mara mbili, ameonekana kuwa na dalili ndogo za ugonjwa huo.

Hata hivyo hiyo haimzuii kuendelea na majukumu yake ya siku zote, na kwamba
atatakiwa kushiriki vikao kwa njia ya simu na Zoom.

Kulingana na Itifaki ya Ikulu ya Marekani, Rais Biden ataendelea kufanya kazi peke yake hadi atakapothibitishwa kuwa hana virusi hivyo.

Mke wa Biden, amepima na hajakutwa na maambukizi ya UVIKO -19.

Katika ujumbe wake kupitia mtandao wa Twitter, Rais huyo wa Marekani amesema anaendela vizuri.