Kongamano la saba la wahandisi wanawake linatarajiwa kufanyika tarehe 29 mwezi huu mkoani Dar es Salaam.
Lengo la kongamano hilo ni kuhamasisha wanawake kuingia katika fani za uhandisi,, pamoja na kutoa fursa za biashara.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa taasisi ya wanawake wahandisi Esther Christopher amesema, kongamano hilo lenye kauli mbiu isemayo Ajirika, Uongozi na Ubunifu kwa Wahandisi Wanawake Tanzania, litafanyika pamoja na utoaji tuzo katika sekta tatu.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo litakalohudhuriwa na washiriki kutoka Tanzania, Zambia, Uganda na Kenya, anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.