Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Camilius Wambura amewaomba Watanzania wote hasa wakazi wa jiji la Arusha kushirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wahalifu na wale wote wenye nia ya kuchafua taswira nzuri ya nchi.
Amesema Jeshi la Polisi limejipanga vema kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo nchini hasa wakati huu wa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), unaofayika jijini Arusha.
IGP Wambura ameyasema hayo jijini Arusha wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki , ambao wakuwa na mkutano wao jijini humo hapo kesho.