Manara apigwa stop kujihusisha na soka

0
110

Msemaji wa Yanga, Haji Manara amefungiwa miaka miwili kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi na pia atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 20.

Manara amekutwa na hatia ya makosa ya kimaadili na kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kutofautiana na Rais wa shirikisho hilo Wallace Karia wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Julai 2, mkoani Arusha.