Shehena ya meno ya tembo yakamatwa

0
156

Maafisa nchini Malaysia wamekamata shehena ya meno ya tembo, magamba ya kakakuona na nyara mbalimbali, zikiwa na thamani ya dola milioni 18 za Kimarekani huku vitu hivyo vikielezwa kuingizwa nchini humo vikitokea Barani Afrika.

Idara ya Ushuru wa Forodha nchini Malaysia imesema, wamekamata shehena hiyo ikihusisha pia mafuvu na mifupa ya wanyamapori, vitu ambavyo vilikuwa vikisafirishwa kwenye kontena.

Shehena hiyo yenye uzito wa tani sita inadaiwa kuingizwa nchini huko kwa meli ikitokea Abu Dhabi katika Umoja wa Falme za Kiarabu.