Raia wa China ashtakiwa kwa makosa ya kusafirisha watoto

0
193

Raia wa China ambaye alinaswa kwenye mkanda wa video akiwafundisha watoto wadogo nchini Malawi kutamka maneno yanayoashiria ubaguzi wa rangi amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka matano ya usafirishaji wa watoto.

Lu Ke ambaye alikamatwa nchini Zambia na kukabidhiwa kwa mamlaka za Malawi ambapo alikuwa akiishi akiwatumia watoto kutengeza video ambazo baadhi zilikuwa na maudhui ya kibaguzi.

Raia huyo ambaye alibainika katika uchunguzi wa BBC amekuwa akitengeza video za watoto wakiimba au kutamka maneno mbalimbali ambazo huuzwa hadi TZS 150,000 kwenye mitandao ya kijamii ya China.

Baada ya kufikishwa mahakamani Julai 18 mwaka huu, jaji alikataa ombi la kupewa dhamana akihofia usalama wake na pia uwezekano wa yeye kutoroka.

Lu Ke alikimbilia nchini Zambia mwezi uliopita baada ya taarifa ya kiuchunguzi ya BBC kuweka hadharani na kuonesha udhalimu aliokuwa akiufanya.