Mtanzania kujiunga na Ajax

0
143

Kijana wa Kitanzania, Giovanni Semaganga maarufu Giovinco, amechaguliwa kujiunga na timu ya Ajax U 15 ya nchini Uholanzi.

Mwezi Agosti mwaka 2021, Giovanni alianza kuchezea timu inaitwa Rinkan SC inayoshiriki ligi ya U11 huko Tokyo, Japan.

Giovanni amechaguliwa na timu hiyo ya Ajax kwa ajili ya kumuendeleza katika mchezo wa soka kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 15.

Anakuwa mchezaji wa pili mdogo kutoka Tanzania kuchukuliwa na timu hiyo baada ya Baraka Seif kufanya vizuri katika medani ya soka katika timu hiyo.