Daktari mbaroni kwa kumdhalilisha mjamzito

0
201

Daktari wa ganzi katika Hospitali ya Wanawake ya Vilar dos Teles, nchini Brazil anashikiliwa na polisi kwa kumdhalilisha kingono mwanamke aliyekuwa akijifungua hospitalini hapo.

Giovanni Bezerra (32) anadaiwa kuwazidishia wagonjwa wake dawa ya usingizi, jambo lililopelekea uongozi wa hospitali hiyo kuweka kamera za kisiri katika chumba cha upasuaji alipokuwemo daktari huyo.

Katika video na picha zilizosambazwa na hospitali hiyo, Bezerra anadaiwa kumfanyia vitendo vya kingono mama huyo mwenye asili ya Kiafrika aliyekuwa akijifungua kwa njia ya upasuaji.

Gavana wa Rio de Janeiro amezungumzia mkasa huo na kusema, “Nilistaajabishwa kufahamu kisa cha kikatili cha daktari wa ganzi katika Hospitali ya da Mulher, huko São João de Meriti, kilichorekodiwa akibaka mgonjwa. Niliamua kwamba kuwe na ukali na kasi katika uchunguzi wa malalamiko haya makubwa. Serikali ya RJ itatoa msaada na usaidizi wote unaohitajika kwa mwathirika.”

Kwa sasa Bezerra ameripotiwa kushtakiwa kwa ubakaji wa mtu aliye katika hali ya uhitaji, adhabu ambayo ni kati ya miaka 8 hadi 15 jela.