Bodi ya TARURA yakagua barabara ya kimkakati

0
156

Wajumbe ya Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) wameendelea na ziara ya ukaguzi wa barabara za Mradi wa Agri-Connect katika Mkoa wa Iringa, hasa wilaya ya Mufindi na kukagua Barabara ya Sawala- Mkonge-Iyegeya yenye urefu wa kilomita 30.3.

Barabara hiyo imejengwa kwa thamani ya Shilingi bioni 8.16

Lengo kuu la Mradi huo imeelezwa ni Kurahisisha usafirishaji wa mazao ya Mboga mboga, Chai, matunda na mazao mengine toka mashambani kwenda mikoa mingine au kwenda Viwandani ama katika maghala ya kuhifadhia mazao.

Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo wamesema Mradi huo pia umeleta faida nyingi za kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa Ajira kwa wananchi wanaoishi wa maeneo ya mradi wakati wa utekelezaji ambapo kiasi cha ajira 470 katika miradi yote zimekwishatolewa.

Faida nyingine ni kusaidia ukuaji wa Uchumi wa maeneo hayo kwa kuimarisha hali ya usafiri, Ukuaji wa Sekta binafsi katika biashara, Uimarishaji wa sekta ya Afya na Upatikanaji wa Chakula kwa ujumla katika maeneo yote yanayozunguka mradi huo.