Kenya walia na kupanda gharama za maisha

0
1220

Wananchi nchini Kenya wamesema serikali mpya itakatoundwa baada ya uchaguzi mkuu wa Rais utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu itakuwa na jukumu kubwa la kutatua matatizo ya wananchi ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha.

Wananchi hao wameyasema hayo wakati wakiandamana kuitaka serikali kuingilia kati, ili kudhibiti kupanda holela kwa bei za bidhaa ikiwemo vyakula na mafuta ya kuendeshea vyombo vya moto.

Wamedai kuwa bei za bidhaa ikiwemo mafuta ya kupikia zimepanda mara dufu na hivyo kufanya maisha kuwa magumu hasa kwa wananchi wa kipato cha chini.