Shinzo Abe kuzikwa leo

0
166

Wananchi wa Japan wanaendelea kuomboleza kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Shinzo Abe, aliyeuawa Ijumaa iliyopita alipokuwa akikifanya kampeni za uchaguzi wa wabunge kwa chama chake cha Liberal Democrat (LDP).

Tayari mwili wa kiongozi huyo umewasili katika hekalu ambapo shughuli za mazishi zinatarajiwa kufanyika mjini Tokyo.

Mazishi ya Abe yanafanyika leo yakihudhuriwa na watu wachache hasa wa familia yake.

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida ameahidi kuzifanyia kazi ahadi ambazo Abe alizitoa wakati wa kampeni, ikiwa ni pamoja na kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo.

Kishida ametoa kauli hiyo baada ya chama chake kujizolea ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika nchini humo siku ya Jumapili.