Mpango wa kuwasaidia wakulima wa pamba waja

0
116

Mrajisi msaidizi wa Tume ya maendeleo ya ushirika Robert Nsunza, amesema tume hiyo inatarajia kuanzisha minada ya kuuza pamba ya wanachama wa vyama vya ushirika nchini.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika viwanja vya sabasaba yanapofanyika maonesho ya 46 ya biashara kimataifa mkoani Dar es Salaam.

Amesema kupitia shirika bei ya pamba sokoni imeongezeka kwani chama hicho kiliweza kupelekea wadau waongeze bei kutokana na ushindani ulioibuka ukiwa umetiwa chachu kwa uwepo wa vyama vya ushirika kwenye soko la pamba.

Sambamba na hilo amesema mpango huo umekuja baada ya kuona mafanikio katika soko la kahawa ambalo iliuzwa kwa mnada na kupelekea bei ya zao hilo sokoni kuwa yenye kuridhisha mwaka huu.

Naye meneja mwendeshaji wa Chama Kikuu cha wakulima Tabora (WETCU 2018 LTD) ameeleza faida anazozipata kutokana na kuwa mwanachama wa vyama vya ushirika nakusema kuwa zipo bidhaa ambazo ni vigumu kuuzika kama muuzaji sio mwanachama wa vyama vya ushirika kwani bidhaa hizo hupata wateja kwa bei za ushindani sokoni.

Kwa upande wake Mariam Msangi
Mwanachama wa chama cha ushirika Madirisha amewashauri wanawake wajasiriamali kujiunga na vyama vya ushirika ili kunufaika na faida zake.