IGP Sirro awahakikishia usalama wawekezaji

0
138

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Siro , amewahakikishia wawekezaji wenye nia ya kufanya shughuli za biashara na uwekezaji nchini kuwekeza bila hofu kwa kuwa Tanzania ni salama na jeshi hilo lipo kwa ajili ya kulinda usalama wa watu na mali zao

IGP Siro ameyasema hayo hii leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa ya Dar es salaam, maarufu sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam ambapo pia ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa wenye nia ovu ya kutaka kutumia mkusanyiko wa maonesho hayo kutekeleza vitendo vya kihalifu.