Shinzo Abe afariki dunia

0
137

Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe amefariki dunia baada ya kupigwa risasi akiwa katika kampeni za chama chake cha Liberal Democratic  (LDP)  kwenye uchaguzi wa wabunge katika mji wa Nara Magharibi mwa nchi hiyo.

Abe amefariki dunia hospitalini baada ya kulazwa akiwa mahututi kufuatia kupigwa risasi ambapo Katibu Mkuu Kiongozi nchini humo Hirokazu Matsuno pamoja na Waziri Mkuu Fumio Kishida wamesema hali ya Abe ilikuwa mbaya baada ya kupata shambulio la moyo.

Tayari mshambuliaji amekamatwa na maafisa wa usalama na walinzi wa Abe muda mfupi baada ya kutekeleza shambulio hilo.

Shinzo Abe ametumikia wadhifa wa Waziri Mkuu wa Japan kutoka mwezi Desemba  mwaka 2012 hadi mwezi Septemba mwaka  2020, hivyo kuwa Waziri Mkuu wa Japan wa kwanza kuwahi kutumikia wadhifa huo kwa muda mrefu zaidi.