Waziri Mkuu wa zamani wa Japan ashambuliwa kwa risasi

0
146

Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe amelazwa hospitalini  akiwa mahututi baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa katika kampeni za chama chake cha Liberal Democratic (LDP), kampeni za uchaguzi wa wabunge katika mji wa Nara magharibi mwa nchi hiyo.

Katibu Mkuu Kiongozi wa Japan, Hirokazu Matsuno pamoja na Waziri Mkuu Fumio Kishida wamesema hali ya Abe ni mbaya baada ya kupigwa risasi na kupata shambulio la moyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken na Balozi wa nchi hiyo nchini Japan, Rahm Emanuel wamesema tukio hilo linapaswa kulaaniwa huku baadhi ya wakosoaji wakilaumu mfumo dhaifu wa ulinzi ambao umemwezesha kumshambuliaji kumpiga risasi kiongozi huyo kifuani na shingoni huku akiwa karibu naye.

Mshambuliaji huyo amekamatwa na maafisa wa usalama na walinzi wa Abe muda mfupi baada ya kutekeleza shambulio hilo.

Shinzo Abe ametumikia wadhifa wa Waziri Mkuu wa Japan kutoka nwezi Desemba mwaka 2012 hadi Septemba  mwaka 2020, na hivyo kuwa Waziri Mkuu wa Japan kuwahi kutumikia wadhifa huo kwa muda mrefu.