Gharama za ujenzi hospitali Ukerewe kizungumkuti

0
98

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa ya wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, ambapo pamoja na mambo mengine ametaka kufahamu gharama halisi za ujenzi wa mradi huo.

Katika ziara hiyo aliyofuatana na Mhandisi wa wizara ya afya Paulo Koloso, Dkt. Mollel ametaka kufahamu uhalisia wa gharama hizo kutoka kwa mhandisi huyo, mhandisi wa Mkoa na wa wilaya ambao walipishana katika kuelezea gharama.

Naibu Waziri Mollel alimuuliza Mhandisi wa Wizara kwanini mradi huo umekua na gharama kubwa na haukua na uokoaji wowote wa fedha lakini Mhandisi Koloso alimjibu kwa jazba kuwa anasimamia taaluma na kwamba yuko tayari kufukuzwa kazi kitendo ambacho kilimuudhi mkuu wa wilaya na kuamuru OCD amuweke ndani.

Miongoni mwa vitu vilivyohojiwa na Dkt .Molel ni pamoja na toilet paper holder iliyopangwa kununuliwa kwa shilingi laki tano.