Mene: Litumieni soko huru la Afrika

0
143

Katibu mkuu wa eneo huru la biashara Afrika Wamkele Mene amefungua Rasmi maonesho ya biashara ya 46 ya biashara kimataifa ya Dar es Salaam maarufu sabasaba ambapo ametoa rai kwa wazalishaji wa bidhaa za Afrika kutumia eneo huru la biashara Afrika ili kusaidia kukuza uchumi wa Afrika unaokadiriwa kuwa na pato ghafi lenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 3.4

Akifungua maonesho hayo baada ya kutembelea mabanda ya bidhaa za wafanyabiashara na wajasiriamali katika maonesho hayo hii leo Katibu mkuu wa eneo huru la biashara Afrika Wamkene Mene amesema ni wakati waafrika wakaanzisha soko la Afrika kwa kuuziana bidhaa bila kuathiri masoko mengine ya kimataifa .

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji wamesema Tanzania imedhamiria kufungua milango ya kibiashara na kuimarisha diplomasia ya uchumi na pia ipo tayari kushiriki kikamilifu kwenye soko huru la Afrika.