Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Jacob Mkunda amesema
Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) limeendelea na shughuli za uzalishaji mali wa faida, ili kuipunguzia serikali gharama ya malezi ya vijana wanaojiunga na Jeshi la kujenga Taifa kupitia kampuni zake tanzu na viwanda mbalimbali.
Jenerali Mkunda ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutimiza miaka 41 tangu kuanzishwa kwa SUMA JKT.
Amesema mbali na SUMA JKT kuipunguzia serikali gharama ya kuendesha Jeshi la Kujenga Taifa, pia shirika hilo limekuwa likichangia pato la Taifa kwa kutoa gawio na kodi, kutokana na bidhaa na huduma zinazozalishwa.