Hospitali za mikoa zapigwa stop matumizi ya fomu za 2C

0
180

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesitisha matumizi ya fomu ya Bima ya Afya (NHIF) ya kununulia dawa nje ya kituo cha kutolea huduma za afya (FORM 2C) kwa Hospitali zote za Rufaa za Mikoa.

Waziri Ummy ametoa maelekezo hayo leo baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi na kuangalia hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru katika Mkoa wa Arusha

“Kuanzia jana Wizara ya Afya imesitisha matumizi ya fomu ya Bima ya Afya ambayo mgonjwa akifika hapa Hospitali na hakuna dawa anaandikiwa ile fomu akanunue kwenye maduka binafsi ya dawa” amesema Waziri Ummy Mwalimu

Amesema sio kazi ya mgonjwa kutoka nje kwenda kutafuta dawa na kuwataka watendaji ndani ya Hospitali kuhakikisha dawa zipo na zinapatika wakati wote na endapo hazipo wachukue wajibu wa kwenda kuzitafuta na kumpa mgonjwa.